15 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Binti adaiwa kutoroshwa na ticha wake Mganda
 
2007-06-15 16:17:50
Na MAABAD MSUYA, MIKOCHENI

Mama mmoja wa Ki-Zanzibari amethibitisha kauli ya kuwa `uchungu wa mwana aujuaye mzazi` baada ya kusafiri toka kwao `Zenji` hadi Dar kwa nia ya kuhitaji msaada wa kumpata bintiye wa miaka 16 ambaye tetesi zinasema ametoroshwa visiwani humo na mwalimu wake mmoja wa darasa.

Mama huyo aliyejawa na uchungu uliomfanya atinge kwenye ofisi hizi juzi, amejitambulisha kwa jina la Bi. Bishara Haroub.

Bi. Bishara anasema ametua Jijini kwa nia moja tu ya kuhitaji msaada wa namna yoyote ile katika kumpata bintiye aitwaye Bi. Mariam Farid.

Akizungumza na Alasiri, Bi. Bishara amesema binti yake huyo ana mwezi wa nne sasa tangu atoweke kwao.

Akasema mtu anayemuhisi kuwa ndiye aliyemtorosha bintiye ni mwalimu mmoja wa kiume pale katika shule moja ya sekondari binafsi ambako bintiye Mariam alikuwa akisoma kidato cha pili.

`Naomba yeyote atakayemuona anisaidie kumpata mwanangu… hadi sasa sina taarifa zake. Sijui kama ni mzima au vinginevyo,` akasema Bi. Bishara huku akibubujikwa machozi.
Akasema anaiomba Serikali imsaidie katika harakati za kumpata mwanawe, ambaye anadhani ametoroshwa kwao na mwalimu wake huyo wa Mganda.

Akisimulia zaidi, Bi. Bishara amesema mwanawe alitoweka tangu Februari Nane mwaka huu, mishale ya saa 2:30 asubuhi baada ya kutoonekena darasani kwao.

Hatahivyo, Bi. Bishara akabainisha kuwa yeye na familia yake walitaarifiwa habari hizo za kupotea kwa Mariam mnamo Februari 21 mwaka huu, hivyo kuingiwa na hofu juu ya namna suala hilo lilivyoshughulikiwa na uongozi wa shule hiyo ya bweni aliyokuwa akisoma binti yake.

`Tayari tumesharipoti suala hili kwenye vyombo husika… tunachoomba sasa ni kusaidiwa namna ya kumpata Mariam,` akasema Bi. Bishara, ambaye ana nakala za barua kadhaa zinazoonyesha jitihada za familia yao katika kumsaka binti huyo.

Akaomba yeyote atakayebahatika kumuona Mariam awasilishe taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu naye.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.