16 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

`Wananchi Misungwi sasa jikwamueni`
 
2007-06-16 18:26:29
Na Aziz Issa

Serikali imetenga dola 802,052 za Marekani (Sawa na Sh. 982,462,400) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Pesa hizo zitatumika kwa ajili ya miradi mbalimbali itakayoibuliwa na jamii kwa kipindi cha miradi kitakachomalizika mwezi Desemba 2009.

Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Bw. Gaudence Kayombo ameliambia Bunge mjini Dodoma kuwa fedha hizo zimetolewa kwa wananchi wa wilaya ya Misungwi, kupitia Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF)

Akasema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2006 hadi Aprili 2007, wilaya ya Misungwi iliidhinishiwa Sh. 362,496,413 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 11 na tayari imeshapewa Sh. 175,907,349 kwa awamu ya kwanza.

Amesema mpaka saa vijiji 11 tayari vimeshanufaika na fedha hizo kwa kupewa jumla ya Shilingi 362,496,413 kupitia TASAF.

Akasema fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuboresha ufugaji ng’ombe, ujenzi wa soko, barabara na ujenzi a vyumba vya madarasa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.