16 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kijana anayedaiwa kibaka Jijini apigwa hadi kufa
 
2007-06-16 18:27:11
Na Job Ndomba, Kinondoni

Kijana mmoja anayedaiwa kuwa ni kibaka amefariki dunia baada ya kupata kipigo kikali toka kwa wananchi wenye hasira.

Kamanda wa mkoa wa kipolisi Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow , ameiambia Alasiri kuwa tukio hilo limegundulika mishale ya saa 1.30 asubuhi jana, ikiwa ni baada ya wananchi kutoa taarifa ya kuonekana kwa kijana huyo akiwa taabani pale Mwananyamala.

Amesema Kamanda Rwambow kuwa baada ya kufika eneo la tukio, polisi walimkuta kijana huyo akiwa hoi kutokana na kipigo kinachodaiwa kuwa amekipata toka kwa wananchi wenye hasira.

Hatahivyo, haikuelezwa ni kitu gani alikwapua kijana huyo hadi wanaanchi hao wakaamua kumpiga hadi akakutwa na umauti.

Bw. Rwambow amesema kabla ya kifo chake, kijana huyo aliweza kujitaja jina moja la Juma na kwamba makazi yake ni Tandale Jijini.

Akasema marehemu alifariki njiani wakarti akiwahishwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Kamanda Rwambow amewataka wananchi waende kuutambua mwili wa kijana huyo pale katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Mwananyamala Jijini.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.