16 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Asasi binafsi zatakiwa ziache kufanya kazi `kisanii`
 
2007-06-16 18:29:43
Na Futuna Seleman, Jijini

Serikali imezitaka asasi zisizo za kiserikali, zinazojihusisha na masuala ya vijana nchini
kuhakikisha kuwa zinafanya kazi zao kwa mujibu wa malengo yao na si kuandika miradi ya kuwafanya wajinufaishe wenyewe.

Naibu Waziri wa Kazi, ajira na Maendeleo ya Vijana, Bw. Emmanue Nchimbi, amesema hivi sasa kumeibuka asasi nyingi ambazo ofisi zake ziko kwenye `briefcase`, hali ambayo huwakatisha tamaa vijana.

Naibu Waziri huyo, ameyasema hayo wakati anafunga warsha, iliyokuwa ikizungumzia masuala ya uzazi, vijana na ugonjwa wa ukimwi, iliyoandaliwa na AMREF.

Pia taasisi hiyo ilikuwa ikitimiza miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwake.

`Fanyeni kazi karibu na vijana. Ni vizuri taasisi zenu zikashirikiana na Serikali kama ilivyo AMREF,` akasema Naibu huyo.

Akasema Serikali itatoa ushirikiano na kamwe haitapuuza juhudi zinazofanywa na asasi binafsi zinazofanya kazi zake kwa utaratibu unaotakiwa.

Aidha, Naibu Waziri Nchimbi akasema Serikali inasimamia uundwaji wa Baraza la Vijana la Taifa ambapo tayari baraza la mawaziri limeshalipitisha

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.