16 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Majambazi Dar yadakwa bar, moja lauawa
 
2007-06-16 18:30:32
Na Job Ndomba, Temeke

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hatari wamedakwa kiulaini na polisi wakati wakiwa wamelewa chakari bar huku mwingine akitandikwa risasi katika tukio moja lililofeli kule Temeke Jijini.

Kamanda wa mkoa wa kipolisi Temeke, Emmanuel Kandihabi, ameiambia Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi kuwa matukio hayo yamejiri jana.

Kamanda Kandihabi amelitaja tukio la kwanza kuwa ni lile lililotekea mishale ya saa 8.00 usiku pale kwenye bar moja maarufu inayojulikana kama Sugar Ray ambapo majambazi hayo matatu yalikuwa yakipata kinywaji.

Amesema wakati huo Polisi ilifanikiwa kukamata majambazi mawili na jingine moja kati yao likafanikiwa kutimka.

Akasema baada ya muda mfupi, hilo lililotimka nalo likadakwa na vijana wake shupavu.

Kamanda Kandihabi amesema Polisi ilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa, kwenye baa hiyo kuna majambazi yanapata kilevi na ndipo Polisi walipofika hapo na kufanikiwa kuwadaka.

Aidha, Kamanda Kandihabi amesema baada ya kuwapa kibano kikali, majambazi hao ambao wakamtaja mwenzao ambaye naye alidakwa nyumbani kwake na kukutwa na bastola moja na risasi 13.

Kamanda Kandihabi amewataja majambazi hao kuwa ni Juma Mwita Shabani, Chacha Mwita,30 na Joseph Mwita, 25, ambao wote wanasadikiwa kuwa ni ndugu.

Katika tukio jingine, jambazi moja limeuawa kwa kupigwa risasi likiwa na wenzake wanne baada ya kuvamia kwa nia ya kuiba katika nyumba ya Afisa mmoja wa TASAF, Bw. Kanisius Nkwera.

Kamanda Kandihabi amesema tukio hilo limetokea jana, mishale ya saa 2.15 usiku pale Tuangoma ambapo majambazi hayo yalijitoma ndani ya nyumba ya Bw. Nkwera na kutaka yapewe fedha.

Bw. Kandihabi ameiambia Alasiri kuwa majambazi hayo yaliingia hapo kwa kupitia mlango wa nyuma wa nyumba hiyo na kumkuta mfanyakazi wa ndani, Bi. Mariam Dotto,19 ambapo walimuweka chini ya ulinzi na kumtaka atoe fedha.

Baada ya kumpa kibano binti huyo alitoa Sh.56,000, lakini hawakuridhika na kuingia sebuleni ambako walimkuta baba mwenye nyumba akiangalia Tv na kumpa kipigo ambapo naye alitoa Sh. 60,000, lakini hawakuridhika.

Akasema baada ya hapo, Bw. Nkwera akawazdi ujanja na kumtwanga risasi mmoja wao, baada ya kuwahadaa kuwa anafuata pesa, kumbe akarejea na bastola.

Akasema majambazi wengine walilazimika kiutimua mbio baada ya kuona wamewahiwa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.