16 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Konda wa daladala Jijini apigwa risasi
 
2007-06-16 18:33:07
Na Futuna Selemani, Temeke

Kondakta wa daladala lisilofahamika, Bw. Mandela Peter Njau, amepigwa risasi mguuni wakati wa ugomvi kati yake na abiria.

Kamanda wa mkoa wa kipolisi Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi, ameimbia Alasiri kuwa tukio hilo limejiri mishale ya saa 5.15 huko maeneo ya Keko Magulumbasi Jijini.

Kamanda Kandihabi amesema kijana huyo anadaiwa kupigwa risasi na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Associate Engineering, Bw. Saidi Issa Zullu.

Akasema kwa mujibu wa majeruhi huyo, ni kwamba alipigwa risasi wakati akipita mbele ya gari ya mkurugenzi huyo akielekea kwenye gari alilokuwa akifanyia kazi.

Aidha, amesema Mkurugenzi huyo naye amesema alimpiga risasi dereva Njau kwa bahati mbaya baada ya kutaka kujihami wakati alipokuwa akipita nje ya ofisi yake na kukuta ugomvi mzito kati ya abiria na kondakta huyo.

Akasema kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, wakati wa tukio, yeye alikuwa na mkoba wenye nyaraka mbalimbali pamoja na fedha taslim zaidi ya milioni moja.

Imeelezwa kuwa alipofika eneo la ugomvi, bahasha iliyokuwa na fedha ikaanguka baada ya kuvutwa begi lake na mtu asiyefahamika na katika kuzuia asiibiwe, ndipo alipofyatua bastola yake.

Bw. Kandihabi amesema majeruhi yupo katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili na mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa upelelezi zaidi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.