21 Aug 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanaoishi na VVU Manzese wajazwa mapesa
 
2007-08-21 16:38:37
Na Abdul Mitumba, Manzese

Wanawake 30 wanaoishi na virusi vya Ukimwi katika kata ya Manzese, Manispaa ya Kinondoni wamepata msaada wa sh. 50,000 kila mmoja kwa ajili ya kujianzishia biashara ndogondogo.

Fedha hizo zimetolewa na asasi isiyo ya kiserikali ya Tupendane iliyobeba jukumu la kuwatunza na kuwasaidia wenye VVU katika kata hiyo.

Mwenyekiti wa asasi hiyo, Bi. Aisha Fellix amesema fedha hizo wamezipata kutoka katika mtandao wa kitaifa wa wanaoishi na VVU nchini, HIT.

Amesema, awali asasi yake ilitoa msaada wa fedha hizo watu 15 kabla ya kuwapa wengine 15 jana hivyo kufanya waliofikiwa na msaada huo kuwa 30.

Akasema lengo la msaada huo ni kuwawezesha kuichumi wakazi wa kata hiyo wanaoishi na VVU.

`Sisi kama Tupendane tunaamini kwa kuwasaidia wenye VVU kiasi kidogo kama hicho cha fedha kwa kila mmoja, kinaweza kuwasaidia kuendesha biashara ndogondogo hatimaye kuondokana na umaskini ngazi ya familia,` amesema Bi. Aisha.

Akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo kwa wenye VVU, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Manzese, Bw. Bryceson Mwangomo, aliwataka wahanga hao kutumia vizuri fedha hizo ili kujikwamua na umaskini.

Alisema haitakuwa na maana kama walengwa watatumia fedha hizo kwa shughuli nyingine kwani kufanya hivyo kunaweza kuwaongezea umaskini hatimaye kupoteza matumaini ya kuendelea kuishi na VVU.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.