|
Penzi lazua balaa Dar
2007-08-23 18:35:36
Na Futuna Selemani
Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Rukia Dotto, 30, amejeruhiwa vibaya kwa kufyekwa mapanga na mumewe kutokana na sababu zinazotajwa kuwa ni za wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, amesema tukio hilo lilitokea jana mishale ya saa 10:00 jioni huko Mbagala Kipati Jijini Dar baada ya kuzuka ugomvi baina ya wanandoa hao.
Amemtaja mwanaume aliyefanya unyama huo kuwa ni Bw. Eroismin Lema, ambaye alikimbilia kusikojulikana baada ya tukio hilo na sasa polisi wanamsaka kwa udi na uvumba.
Kamanda Kandihabi amesema Bw. Lema amemfyeka mara tatu mkewe Rukia kwa panga katika mkono wa kushoto na kisha akakiondoa kabisa kiganja cha mkono huo.
Amesema chanzo cha mkasa huo ni wivu wa Bw. Lema ambaye alikuwa akiimtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapaenzi na mwanaume mwingine.
Amesema Kamanda Kandiohabi kuwa hadi sasa, Rukia amelazwa akiwa hoi katika Hospitali ya Temeke na mwanaume huyo bado hajapatikana.
|