23 Aug 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ukuta waua mtu Jijini Dar
 
2007-08-23 18:36:11
Na Mwanaidi Swedi, Kinondoni

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Danni au jina la utani Osama amekufa baada ya kudondokewa na ukuta wakati wakibomoa nyumba.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi, Kinondono Jamali Rwambow, ameliambia alasiri leo asubuhi kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 7:00 usiku huko maeneo ya Manzese Midizini jijini Dar es Salaam.

Kamanda Rwambow amesema mtoa taarifa, Bw. Edwin Mmasi,51, Fundi ujenzi aliiambia Polisi kuwa akiwa Kinondoni, Mtaa wa Karafuuu akiwa anasimamia uvunjaji wa nyumba ya mama Rehema Abdalah, ghafla mmoja wa vibarua wake Bw. Osama aliangukiwa na ukuta na kufa.

Kamanda amesema kuwa Bw. Mmasi alieleza kuwa akiwa kazini na vibarua wake wapatao sita walianza shughuli hiyo ya ubomoaji saa 5:00 asubuhi ilipofika saa 11:00 jioni ndipo ukuta ulipondoka.

Kamanda amesema kuwa walielezwa kuwa nyumba hiyo ilikuwa na vyumba vitano ambapo walipokuwa wanamalizia nyumba vitatu kati ya vile vitano ukuta wenye kozi nane ulidondoka na kumuangukia kijana huyo.

Aidha kamanda amesema baada tu ya kumdondokea ukuta ule vibarua wenzake walifanya jitihada za kumuokoa na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala na baadaye alikufa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhiwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.

Wakati huo huo, Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni amesema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Salum Abdallah, 26, amejinyonga na kufa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.