23 Aug 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Zitto: Kazi ipo...JK atua kwenye ngome yake
 
2007-08-23 19:07:41
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete ametinga kwenye mgodi wa madini wa Buzwagi ambao hivi sasa watu wanauita kama `Ngome ya Zitto`.

Jina hilo limeibuliwa kutokana na ukweli kuwa sakata la mgodi huo, ndilo lililomfanya Mheshimiwa Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) apigwe stopu kushiriki vikao vya Bunge.

Ziara hiyo ya Rais Kikwete katika mgodi wa Buzwagi, ni sehemu ya ziara yake ya Kiserikali ya siku nane mkoani Shinyanga.

Rais Kikwete ametembelea mgodi huo na kujionea shughuli zinazoendelea kufanyika hapo ikiwa ni siku chache tu baada ya Mhe. Zitto kusimamishwa bungeni kutokana na matamshi yake kuwa Waziri Karamagi amedanganya kuhusu mkataba aliosaini na kampuni inayoendesha mgodi huo.

Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili wamesema Rais amekwenda huko ili `kupata nyepesi nyepesi’ juu ya vuguvugu lililosababishwa na sakata la Mhe. Zitto.

Akiwa ziarani kuelekea kwenye eneo la mgodi huo, wananchi wa Buzwagi waliusimamisha msafara wake na kutaka kuzungumza naye.

Hata hivyo hawakuzungumzia lolote kuhusu sakata la Zitto na badala yake wakaelezea matatizo kadhaa ya kijamii yanayowakabili.

Akizungumza na wananchi hao, Rais Kikwete aliwaahidi kuwa kutokana na uwekezaji huo wataweza kupata huduma za kijamii kama vile maji, shule na umeme.

Akasema mgodi huo utakapoanza kufanya kazi, utasaidia kuinua uchumi na kuleta maisha bora kwa wakazi wanauzunguka.

Hivi karibuni, Bw. Zitto aliwasilisha hoja binafsi bungeni, akitaka iundwe kamati teule ya bunge kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa mkataba huo.

Hata hivyo Mbunge huyo aliishia kusimamishwa kujihusisha na shughuli za Bunge kwa madai kuwa amemsingizia kusema uongo Waziri Nadhir Karamagi ambaye ndiye mwenye dhamana ya Nishati na Madini.

Hatua hiyo ilisababisha watu mbalimbali wakiwwemo wanaharakati kuja juu na kuandamana kupinga hatua hiyo ya kusimamishwa kwa Mhe. Zitto.

Hata hivyo yeye mwenyewe ameapa kupigana kiume hadi ukweli wa jambo hilo ufahamike.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.