25 Aug 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanafunzi nchini watakiwa kuchangamkia kozi za uhandisi
 
2007-08-25 19:19:12
Na Mariam Mkumbaru, Jijini

Tatizo la uhaba wa wakandarasi linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya miundombinu ambayo ndio chachu ya kukua kwa uchumi wa nchi.

Hayo yalisemwa na Mhandisi Mkuu Bw. Ninatubu Hema, katika maadhimisho ya miaka mitano ya wahandisi yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Bw. Hema amesema kuwa mpaka sasa nchi ina wahandisi 7000 tu, kitu ambacho kinachangia kurudisha nyuma mambo mengi ya maendeleo kama upatikanaji wa maji, umeme, barabara na majengo mbalimbali.

``Tunatoa wito kwa vijana mbalimbali kusomea fani ya uhandisi ili kuweza kuwa na wanataalamu wa mambo mengi yanayohusu uhandisi hapa nchini,`` akasema Bw. Hema.

Amesema kwa sasa wanahitaji wahandisi 7000 wahitimu masomo ya fani hiyo kila mwaka ili kuweza kuwa na wataalamu wa kutosha, ambao watashughurika na nyanja mbalimbali za maendeleo ya miundombinu nchini.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Miundombinu Bw. Makongoro Mahanga, amesema bila nchi kuwa na wahandisi wa kutosha, kamwe hakutakuwa na maendeleo ya kweli.

Bw. Mahanga akasema kuwa wizara yake iko tayali kuwapa mafunzo kwa vitendo wanafunzi wanaotoka katika vyuo mbalimbali ili wawe na uwezo wa kutosha kwenye kazi za kujenga taifa.

Kwa upande wake Msajili wa bodi ya Wahandisi nchini, Bw. Steven Mlote amesema bodi yake kwa sasa inakabiliwa na changamoto za kuwa na uhaba wa vitendea kazi kama magari ya kuzunguka kukagua majengo nchi mzima.

Bw. Mlote akatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika mambo mengi yanayohusu uhandisi, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye bodi yake kwa mambo mbalimbali yanayohitaji huduma za kihandisi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.