25 Aug 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

DAWASCO yawacharukia waosha magari Dar
 
2007-08-25 19:19:57
Na Kiyao Hoza, Jijini

Watu wanaotoa huduma ya kuosha magari Jijini pamoja na wale wanafanya shughuli za kilimo cha bustani za mboga ni miongoni mwa waharibifu wakubwa wa mitandao ya maji ambao sasa watasakwa kwa udi na uvumba ili kuzuia uharibifu huo.

Afisa uhusiano wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka Jijini, DAWASCO, Bi. Badra Masoud, amesema watu hao watasakwa kutokana na uharibifu huo pamoja na wizi wa maji unaosababisha wateja wao halali kukosa maji.

Akasema mara nyingi, shughuli hizo hufanyika katika sehemu zenye mabomba yaliyoharibiwa kwa makusudi na hivyo kuathiri usambazaji wa maji katika sehemu mbalimbali za Jiji.

Bi. Badra ameongeza kuwa kutokana na vitendo hivyo baadhi ya wateja wa kampuni hiyo kukosa huduma hiyo kama ilivyokusudiwa.

``Hii inaonyesha kuwa watu hawa si waungwana na wala hawawatendei haki watu wengine wanaopaswa kupata huduma hiyo,`` akasema Bi. Badra.

Amesema hiyo ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa kampeni ya kuwakamata watu wanaotumia maji kwa njia za wizi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.