26 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakulima kuanzisha benki
 
2008-02-26 15:40:36
Na Azizi Issa

Mtandao wa wakulima wa Dunduliza, unatarajia kauanzisha benki ya mazao kwa lengo la kuwasaidia wakulima kupata mikopo ya fedha na pembejeo.

Mshauri wa Kilimo wa mtandao huo, Bw. Rodgers Masha amesema jambo hilo litawasaidia kunufaika na fedha na pembejeo, jambo ambalo linamekuwa likizishinda taasisi za kifedha kwa sababu ya hofu ya kuogopa kutorejeshewa fedha zao.

Akasema kuanzishwa kwa benki hiyo kutawanufaisha wakulima wengi na kuwaondolea tatizo la ukosefu wa soko kwa mazao na pembejeo.

Pia akasema kuanzishwa kwa benki hiyo kutawawezesha wakulima kupata mafunzo mbalimbali yanayohusika na kilimo.

Akasema tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika wilayani Mbarali mkoani Mbeya zimeonyesha wakulima hawazalishi kwa tija, jambo ambalo linawafanya kushindwa kufikia malengo waliyoyapanga.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.