26 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mafundi gereji wa Kinondoni wachongeana kwa Kandoro
 
2008-02-26 15:41:38
Na Robert Temalilwa, Tegeta

Mkuu wa Mkoa wa Dar Bw. Abbas Kandoro, ameombwa awatimue mafundi gereji wote wenye gereji bubu ambao wamejazana katika mitaa mbalimbali ya manispaa ya Kinondoni na kuwahamishia katika eneo rasmi walilotengewa na amnispaa yao.

Wito huo umetolewa na Bw. Hamza Matimbwa aliyejitaja kama Mwenyekiti wa mafundi gereji wa Kata ya Kunduchi, wakati alipokuwa akielezea maendeleo ya ujenzi wa gereji katika eneo walilotengewa mafundi wote wa wilaya ya Kinondoni la Asbestos lililopo Wazo Hill, ambako wanaendelea na ujenzi wa gereji zao.

Bw. Matimbwa amesema kuwa hivi sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kumalizia ujenzi wa gereji katika eneo hilo, hivyo Serikali ya Mkoa inapaswa kuwatimua mafundi gereji wote wanaoendelea kufanyia shughuli zao mitaani, katika maeneo yasiyo rasmi.

``Mafundi karibu wote wa Manispaa ya Kinondoni wamepatiwa maeneo katika eneo hili tulilotengewa... lakini kuna ambao bado wapo mitaani. Tunadhani ni wakati muafaka sasa wa kuwaondoa huko kwa nguvu ili wasiendelee kukaidi agizo la Serikali,`` akasema Bw. Matimbwa ambaye amekutwa akiandaa eneo lao na wenzake kadhaa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.