26 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanaouza bidhaa nje ya masoko Kinondoni wachimbwa mikwara
 
2008-02-26 15:47:06
Na Valery Kiyungu, Kinondoni

Muungano wa Masoko Jijini, MUMADA, Kanda ya Kinondoni, umewapa miezi mitatu wafanyabiashara wanaofanyia shughuli zao katika masoko yasiyo rasmi kuacha kufanya hivyo kabla hawajachukuliwa hatua.

Akizungumza na Alasiri ofisini kwake, Mwenyekiti wa MUMADA katika kanda hiyo, Bw. Mohammed Mwenkiya, amesema baadhi ya wafanyabiashara katika Manispaa ya Kinondoni wanaendelea kufanya shughuli zao kwenye masoko yasiyo rasmi na matokeo yake kuwafanya wao wakose wateja.

Akasema ofisi yake imepata taarifa zinazoeleza kwamba baadhi ya wafanyabiashara wamerejea kwenye masoko yasiyo rasmi na hivyo wao hawawezi kuacha jambo hilo liendelee.

``Tunawapa miezi mitatu ya kurejea kwenye maeneo rasmi. Vinginevyo tutaziomba mamlaka husika zichukue hatua kali ikiwa ni pamoja na kuendesha zoezi la kubomoa maeneo yote waliyovamia,`` akasema Bw. Mwenkiya.

Mwenyekiti wa Muungano huo wa Masoko Jijini amesema kuwa uongozi wake umepewa jukumu la kuhakikisha wafanyabiashara wanaendesha shughuli zao katika maeneo yaliyotengwa na Halmashauri ya Jiji, hivyo ameapa kula sahani moja na wafanyabiashara wakorofi.

Bw. Mwenkiya akasema kuwa hivi sasa, kwa sababu wafanyabiashara wenzao wamekuwa wakiendesha shughuli zao kwenye maeneo yasiyo rasmi, wao wamekuwa wakipata hasara kubwa kwa sababu wateja huishia nje na hivyo wao kutofikiwa na wanunuzi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.