26 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ziara ya Rais wa Uturuki yaahirishwa
 
2008-02-26 15:50:56
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Ziara ya Rais wa Uturuki, Abdullah Gui aliyekuwa awasili nchini leo, imeahirishwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Habari, Bw. Salvator Rweyemamu, Rais Gul alitarajiwa kuwa na ziara ya siku mbili nchini kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete.

Amesema Rais Gui alitarajiwa kuwasili nchini na kundi la wafanyabiashara 160 kutoka nchini humo.

``Wakati wa ziara yake, mbali na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, pia alitarajiwa kuhutubia mkutano wa pamoja wa wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki,`` alisema Bw. Rweyemamu katika taarifa yake.

Amesema pia Tanzania na Uturuki zilitarajiwa kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kiufundi, kisayansi na kiuchumi katika eneo la kilimo.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.