17 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mwanaume Dar ajiua kwa kitanzi
 
2008-03-17 19:05:47
Na Usu-Emma Sindila, Jijini

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali alioanza kwa kuutundika mtini kabla ya kujining\'iniza hadi kufa.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow ameiambia Alasiri leo asubuhi kwa njia ya simu kuwa, mtu huyo ametambulika kwa jina la Said Kambawene, 30, fundi maarufu wa baiskeli.

Kamanda Rwambow amesema tukio hilo limetokea jana mishale ya saa 12:00 jioni katika eneo la Makongo Juu.

Amesema marahemu hakuacha ujumbe wowote lakini siku tatu zilizopita, alimsafirisha mkewe kwenda kijijini kwao Mwalusembe katika wilaya ya Mkuranga.

Kamanda Rwambow amesema polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na mwili wa marehemu umehhifadhiwa katika hopsitali ya Mwananyamala.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.