|
Rufaa ya Simba yayeyuka
2008-04-24 17:48:14
By Jacqueline massano, Jijini
Rufaa iliyotarajiwa kukatwa na uongozi wa klabu ya Simba na kupelekwa kwenye mahakama ya michezo ya dunia, CAS, kwa ajili ya kupinga kupokwa pointi imeyeyuka baada ya kuona haitakuwa na mafanikio.
Simba ilikuwa inatarajiwa kukata rufaa hiyo Ijumaa baada ya kuona matokeo yake dhidi ya Polisi Dodoma, na mechi ya Yanga na Kagera Sugar yanawaruhusu kufanya hivyo.
Wekundu hao wa Msimbazi, hawataweza tena kukata rufaa FIFA kwa sababu hata wakifanya hivyo itakuwa kazi bure kwani haitaweza kufikisha pointi ambazo amezipata Yanga
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Simba, ambaye hakutaka jina lake litajwe, timu hiyo haitaweza kutoa tena dola za kimarekani 10,000 kwa ajili ya kukata rufaa ya kurudishiwa pointi tatu.
``Rufaa yetu ilitegemea matokeo ya mechi ya jana, lakini sasa haipo tena sababu ya kukata rufaa,`` alisema.
|