26 Apr 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Machupa aisusa Simba
 
2008-04-26 17:42:19
By Daniel Mkate, Jijini

Licha ya uongozi wa Simba, kuwasamehe wachezaji wake sita iliyowasimamisha kwa madai ya utovu wa nidhamu, lakini mshambuliaji wao mahiri, Athumani Machupa, amesusa kujiunga na kambi ya timu yake inayojiandaa na mechi dhidi ya Yanga hapo kesho, kwa madai ya kuogopa lawama.

Akizungumza na Alasiri jana, Machupa amesema anawashukuru viongozi wa Simba kwa kuona mchango wa wachezaji hao katika timu yao na hata kuwatolea adhabu walizowapa.

``Kwa sasa sioni kama iko haja ya kujiunga na kambi, kwangu ni muhimu nikajiunga baada ya mechi dhidi ya Yanga,`` alisema mchezaji huyo.

``Naipenda Simba kwa moyo wangu, lakini naona kuna lawama mbele yangu kama nitacheza mechi ya Yanga na kushindwa kucheza vizuri.

``Nisingependa kuhusishwa na hujuma, napenda kubaki safi, na hili naweza kulikwepa iwapo nitakuwa mbali na mechi ya Yanga,`` alisema zaidi Machupa.

Machupa amesema pamoja na kusimamishwa kutokana na madai ya utovu wa nidhamu, lakini hana kinyongo na kiongozi yeyote wa timu hiyo kwani ni moja ya majukumu yao ndani ya klabu.

Amesema, licha ya kumalizika kwa msimu wa ligi, lakini bado ni mchezaji halali wa Simba labda hadi hapo uongozi utakapomkana.

``---ndio, mimi bado mchezaji wa Simba hata kama nisipokwenda kambini kujiunga na wenzangu, kwanza muda umekwenda na kesho ndio mechi,`` alifafanua.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.