05 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Idadi ya wazee duniani kuizidi ya watoto, vijana
 
2008-05-05 18:27:21
Na Job Ndomba, Jijini

Idadi ya wazee duniani inatarajiwa kuongezeka na kuzidi ile ya watoto na vijana chini ya miaka 14 kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu ifikapo mwaka 2050.

Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa Jamii katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kitengo cha wazee, Bw. Daniel Masunzu, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha kuhusu elimu ya wazee na ukimwi.

Bw. Masunzu amesema idadi ya wazee duniani kwa sasa inaongezeka sana.

Amesema inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2050, wazee watafikia bilioni 2.

Amesema kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa ya mwaka 1999,kulikuwa na idadi ya wazee wenye umri wa miaka 60 na zaidi wapatao milioni 200 mwaka 1950.

Aidha, ameongeza kuwa idadi hiyo kwa bara la Afrika pekee inategemewa kuongezeka kutoka milioni 38 ya sasa na kufikia milioni 212 ifikapo mwaka 2050.

Hata hivyo, Bw. Masunzu amesema ongezeko hilo ni changamoto kwa Serikali kwa sababu inawajibika kuwa na miundombinu inayopasa kutoa huduma kwa wazee na kwamba hiyo ni nafasi pekee kwa jamii kuongeza kasi ya maendeleo.

Ameongeza kuwa idadi kubwa ya wazee hao ni maskini na katika asilimia 75 miongoni mwao wanaishi vijijini na wengi wao ni wazee wanawake wanaokabiliana na changamoto kubwa za kutunza familia katika hali ya umaskini.

Bw. Masunzu amesema kuwa kuna umuhimu wa Serikali, taasisi na wakala za hiari kuandaa mazingira yanayowatambua wazee na yanayotoa nafasi kwao kushiriki kikamimilifu katika maisha ya kila siku.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.