06 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Moto CCM!
 
2008-05-06 16:12:27
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Moto wa chini kwa chini unazidi kufukuta ndani ya Chama cha Mapinduzi, CCM kufuatia kuibuka kwa makundi yenye misimamo tofauti juu ya nini kifanyike baada ya baadhi ya wanachama wake kuhusishwa na kashfa ya ufisadi.

Taarifa ndani ya chama hicho zinadai kuwa sakata hilo limeleta mgawanyiko mkubwa.

Alipoulizwa juu ya msimamo wa chama kuhusiana na tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi ya wanachama wake vigogo, Katibu Mwenezi wa CCM, Kapteni Mstaafu John Chiligati, amesema wao hufanya kazi zao kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama.

Akasema kwa sababu hiyo, watashughulikia mambo hayo kwa kufuata kanuni hizo za chama, ambazo zimeainisha maadili yanayopaswa kufuatwa na hatua za kuchukua pale inapobidi kufanya hivyo.

``Hawa wanaotuhumiwa si wanachunguzwa? Tusubiri, kama ikithibitika... chama kina maadili yake. Kitachukua hatua kulingana na taarifa za uchunguzi,`` akasema Katibu huyo.

Aidha Kapteni Chiligati ametoa ufafanuzi kuhusiana na tamko lililotolewa na Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) mkoani Tanga, ambalo liliwataka vigogo wote waliokumbwa na kashfa na kujiuzulu nafasi zao serikalini, kuachia pia nafasi nyingine za uongozi ndani ya chama ili kukinusuru na chuki zinazoweza kujengeka kwa umma.

Amesema kwa vile watu hao bado wanachunguzwa, ni vema wanachama wakasubiri matokeo ya uchunguzi.

Tamko la UVCCM Tanga lilitolewa na Mwenyekiti wao, ambaye pia ni Katibu wa Idara ya Uenezi na Siasa mkoani humo, Bw. Emmanuel Kiondo.

Nafasi ambazo UVCCM Tanga walitaka ziachiwe na watuhumiwa ni pamoja na zile za ujumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama, ubunge na uongozi ndani ya kamati mbalimbali za chama ikiwemo ya maadili.

  • SOURCE: Alasiri
Tuma Maoni Yako
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.