07 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Jamii yatakiwa `kuwashughulikia`washirikina
 
2008-05-07 19:42:32
Na Job Ndomba, Jijini

Jamii imetakiwa kuhakikisha kuwa ukatili dhidi ya wazee kwa visingizio vya uchawi unakomeshwa mara moja na pia hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wanaobainika kuwanyanyasa wazee kwa imani zao hizo potofu.

Ushauri huo umetolewa na Afisa ustawi wa jamii kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kitengo cha wazee Bw. Daniel Masunzu wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari kuhusu sera ya wazee nchini.

Bw. Masunzu amesema kuwa jamii ina wajibu wa kuhakikisha wazee wanapata haki zao za msingi pamoja na kuchukua hatua zinazostahili ikiwemo kuwalinda dhidi ya ukatili unaofanywa kutokana na visingizio vya mila potofu.

Aidha, amesema kuwa jamii inapaswa kuzikubali haki za binadamu na faida ya kuwa na wazee katika maendeleo ya taifa.

Sanjari na hayo jamii pia imetakiwa kufanya maandalizi kwa vijana ambao ndio wazee wa baadaye ili kuliwezesha taifa kutokuwa na wazee wanaokula `unga` .

Ameongeza kuwa masuala ya wazee ni mtambuka hivyo wadau pamoja na Serikali inatakiwa kushiriki katika mchakato mzima wa kuboresha maisha ya wazee.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.