08 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Waliolipwa fidia ili wahame maeneo yasiyo rasmi K`ndoni kubomolewa
 
2008-05-08 14:44:38
Na Francisca Jeremiah, Kinondoni

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kinondoni ambao wanaishi katika maeneo yasiyo rasmi, na kulipwa fidia na manispaa ili wahame, wametakiwa kuondoka mara moja kwani zoezi la kubomnoa majumba yao liko mbioni kutekelezwa.

Aidha, wakazi hao ambao tayari wameshapokea malipo kwa ajili ya fidia, wametakiwa kufanya hivyo ili kupisha utekelezaji wa mipango ya utumikaji rasmi wa maeneo hayo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Madiwani wa Halmashauri hiyo, Bw. Ignas Mwitura, wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha bajeti cha Baraza la Madiwani.

Akasema halmashauri ya manispaa ilishalipa fidia kwa wakazi hao tangu mwaka 2006 na hivyo inashangaza kuwaona wahusika wakiendelea kuishi kwa maeneo hayo waliyotakiwa kuyahama mara tu baada ya kupokea malipo ya fidia.

``Kuna baadhi ya maeneo katika manispaa yetu yamejengwa hovyo kabisa... utakuta shule za msingi zipo karibu na gesti, zahanati zimezungukwa na kumbi za muziki na maeneo ya uuzwaji vilevile. Kupunguza tatizo hilo, tukaamua kuwalipa wahusika ili wayaache maeneo hayo lakini inashangaza kuwaona bado wakiendelea kuishi pasi na dalili za kuhama,`` akasema Katibu huyo.

Akasema manispaa imewafumbia macho wahusika kwa muda mrefu ili waweze kuondoka wenyewe kwa utaratibu usiohusisha matumizi ya nguvu.

Akasema kuwa sasa, wameamua kubadili mawazo na kuwa tayari kutumia nguvu ili kuhakikisha kuwa watu hao ambao walishapokea malipo wanahama mara moja.

Aidha, Katibu huyo akaomba Baraza la Madiwani litenge fedha katika bajeti yake ya mwaka huu kwa ajili ya kugeuza matumizi ya mabwawa yaliyopo eneo la Mwnanyamala kwa Msisiri na kulifanya kuwa eneo la kutengeneza magari ili kuweza kuwahifadhi mafundi magari kwa kuendeleza shughuli zao.

``Maisha ni magumu mno na tusiwe tunawafukuza watu katika maeneo yao ambayo wanajipatia riziki na kushindwa kuwapeleka sehemu tunazoamini kuwa zinawafaa... sasa naomba baraza hili liangalie uwezekano wa kugeuza matumizi ya mabwawa hayo kwani hayana umuhimu kwa sasa na tuwape eneo hilo vijana,`` akasema Katibu huyo, ambaye ni Diwani wa Kata ya Kibamba.

Wakati huohuo, Baraza la Madiwani limeazimia kujenga hostelo katika shule zake zote za pembezoni mwa mji.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.