09 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Diwani kata ya Kibamba awashukia viongozi wa mtaa
 
2008-05-09 19:18:23
Na Margaret Malisa, PST

Diwani wa Kata ya Kibamba wilayani Kinondoni amewashukia viongozi wa Mtaa wa Kibamba kwa kutohudhuria mkutano muhimu wa maendeleo ya wananchi wao.

Diwani huyo aitwaye Ignas Mwitula amechukua hatua hiyo baada ya kuitisha mikutano ya mara kwa mara ikiwemo ya harambee ya kuchangia ujenzi wa barabara ya Kibamba Mbuyuni na kujikuta akiwa na wajumbe wachache, jambo alilolielezea kuwa ni ukiukwaji wa maadili ya kazi.

``Mnipe orodha ya majina ya wajumbe ambao hawajafika leo ili niwajue, maana naamini kuwa hawa ndio wanaokwamisha maendeleo ya kata yetu,`` akasema diwani huyo.

Nao wananchi waliokuwepo wamemwambia diwani kuwa ni kweli wanakubali uzembe unaofanywa na baadhi ya wajumbe wao.

Pia wakamchenjia diwani huyo kwa kumueleza kuwa hajawahi kuitisha mkutano ili wazungumzie maendeleo ya kata na kero zao na kukiri kuwa wengi wao siku hiyo ni ya kwanza kuitishwa mkutano.

Hata hivyo, diwani Mwitula akasema kuwa suala la kuitisha vikao ni jukumu la Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa na sio jukumu lake, hivyo atamuuliza Mwenyekti huyo ambaye pia hakufika katika mkutano huo kujua ni kwa nini hakutani na wananchi wake kama ilivyo kawaida kwa mwaka mara mbili.

``Suala la kuitisha mikutano ya mara kwa mara na wananchi ni jukumu la Mwenyekiti ... mimi niko juu.

Hata leo sikutakiwa mimi nije hapa, yeye ndiye aliyetakiwa aje anieleze nini mmefanya kwenye hii harambee, hata hivyo msiwe na wasiwasi, nitashughulikia,`` akasema.

Katika harambee hiyo, wananchi hao walichanga shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kibamba Mbuyuni ambayo inahitaji kiasi cha shilingi milioni 17 hadi kukamilika kwa ujenzi wake.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.