|
Moto waunguza nyumba Dar, noti zateketea
2008-05-13 17:51:02
Na Kiyao Hoza, Polisi Kati
Moto umezuka ghafla kwenye nyumba moja na kuteketeza vitu mbalimbali vyenye thamani ya mamilioni pamoja na pesa taslimu zaidi ya shilingi laki tatu.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Jamal Rwambow, amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12:00 asubuhi huko Ubungo Kibangu.
Kamanda amesema moto huo ulizuka kwenye nyumba iliyokuwa inamilikiwa na Bw.Jackson Matitu, 43, ambaye ni karani wa kampuni ya TICS.
Amesema vyumba hiyo ilikuwa na vyumba vinne ambapo moto huo uliteketeza chumba kimoja kati ya hivyo na kusababisha hasara ya mali ya shilingi milioni 25 pamoja na pesa taslimu shilingi 320,000.
Kamanda amesema kuwa hakuna madhara kwa binadamu kwani wakati moto huo unazuka watu wote hawakuwepo.
Hata hivyo amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
|