14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

TMK kupeleka rufaa kamati ya nidhamu
 
2008-05-14 15:20:19
By Onesmo Kapinga, Jijini

Uongozi wa chama cha soka wilaya ya Temeke, TEFA, leo wanatajarajia kuwasilisha rufaa kwa kamati ya nidhamu kupinga kupokonywa ushindi walioupata dhidi ya timu ya mkoa wa Mbeya, Mapinduzi Stars, katika mashindano ya Kombe la Taifa, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini.

Temeke wameondolewa katika mashindano hayo, baada ya Mapinduzi Stars kukata rufaa kuwapinga wachezaji Sammy Kessy na Rashid Gumbo ambao wanadaiwa walikuwa ni wachezaji wa Mtibwa Sugar na kisha kucheza soka la kulipwa Umangani.

Akizungumza na Alasiri jana jioni, Mwenyekiti wa chama chicho Peter Mhinzi amesema rufaa hiyo, inatarajiwa kukabidhiwa mchana kwa mwenyekiti wa kamati hiyo Said El Maamury ili aweze kutoa haki.

Mhinzi amesema kitendo cha kamati ya mashindano iliyopo chini ya Jamal Bayser kuwanyang`anya ushindi huo hawakubaliani nao kutokana na wachezaji hao kuwa wakazi wa Temeke na kucheza ligi ya wilaya hiyo.

Mhinzi amesema Kessy ambaye amesajiliwa na Mtibwa Sugar katika ligi ndogo katika msimu uliopita na uongozi wa timu hiyo ulimfukuza hivyo mchezaji huyo kubakia huru, ambapo Gumbo wameshindwana na klabu hiyo.

Amesema wachezaji hao wamechezea klabu zao za `uswazi` za Berlin na Fahari katika ligi ya TFF, hivyo kanuni za mashindano hayo wachezaji hao ni halali kuchezea timu yao ya mkoa wa Temeke.

Mhinzi amesema kitendo walichotumia ni cha kiuonevu na hawakubaliana nacho hata iweje.

Katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita, Temeke iliitoa Mapinduzi Stars kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka 2-2 ndani ya dakika 90.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.