|
Yanga fc nao wachokozana
2008-05-14 15:21:16
By Onesmo Kapinga, Jijini
Wanachama wa klabu ya soka ya Yanga wamemwashia `moto` Katibu Mipango ya Klabu hiyo, Patrick Fata na kumtaka ajiuzulu wadhifa wake.
Wanachama hao wanataka kiongozi huyo ajiuzulu kwa vile ameshindwa kutimiza majukumu yake kama kiongozi.
Akiongea kwa niaba ya wanachama wenzake wanaotaka mabadiliko hayo, Haruna Athuman (0176) , alimtuhumu kiongozi huyo kushindwa kuleta maendeleo klabuni hapo.
``Hakuna mipango ya maendeleo klabuni, anafanya nini sas? kwanini asijiuzulu?`` alihoji mwanachama huyo.
Athuman alisema kuwa wanachama wanashangaa kuona Fata anafanya kazi za uhazini wakati ni kinyume na utaratibu.
|