14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kaduguda kufikishwa kortini
 
2008-05-14 15:22:34
By Badru Kimwaga,Jijini

Siku moja baada ya Mwina Kaduguda kusimamishwa wadhifa wa Ukatibu Mkuu klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, uongozi wa klabu hiyo unatarajia kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa fedha.

Viongozi wenzake wanamtuhumu Kaduguda kuchota pesa za posho za wachezaji wakati timu ilipokuwa Msumbiji kwa ajili ya mechi ya Ligi ya mabingwa.

Mohamed Mjenga, Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo ameiambia Alasiri jana kuwa wamefanya uchunguzi na kubaini kuwa Kaduguda alichukua fedha hizo.

``Tutamfikisha mahakamani, ana kesi ya kujibu,`` alisema zaidi.

Amelalamikia Kaduduga kuwa na tabia zisizoendana na maadili ya uongozi, pamoja na kamati ya utendaji ya klabu hiyo kumuonya mara kwa mara.

Hata hivyo jitihada za kumsaka Kaduguda kueleza tuhuma zinazoelekezwa kwakehizo hazikuweza kupatikana baada ya simu yake kutopatikana.

Wakati huo huo, baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wamefurahishwa na hatua ya viongozi wao kumsimamisha Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Mwina Kaduguda kwa utovu wa nidhamu wakidai huo ni mwanzo wa safari ya `kuisafisha` Simba.

Wakizungumza na Alasiri wanachama hao wamesema hawaoni kitu cha ajabu kwa Kaduguda kusimamishwa kwani hakuwa mfano wa kuigwa kwa tabia zake walizoziita zisizo za kiungwana.

Mwanachama mwingine Issa Masharubu, amesema kwa upande wake amepokea kwa mikono miwili maamuzi ya kamati ya utendaji ya klabu hiyo juu ya adhabu waliomchukulia Kaduguda ili iwe fundisho kwa wengine.

Naye mmoja wa viongozi wa klabu hiyo (jina kapuni) amedai kuwa hatua waliyofikia ya kumsimamisha `Simba wa Yuda` imetokana na mwenzao kujisahau.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.