14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakulima Rukwa wanolewa
 
2008-05-14 15:58:55
Na Azizi Issa

Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imeanza mpango kabambe wa kutoa mafunzo kwa wakulima ili kuwaondoa katika kilimo kisicholeta tija.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa halamashauri hiyo, Bw. Antony Mwambene mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa kuendesha mafunzo ya shamba darasa katika vijiji vyote 169.

Akasema wilaya hiyo ina mabwana shamba wapatao 45 jambo ambalo halitoshelezi mahitaji ya wakulima wanaohitaji huduma yao ili kuondokana na kilimo duni.

Akasema halmashauri hiyo ina jumla ya vijiji 169 na kwamba mafunzo hayo yanaendeshwa kwa sasa katika vijiji 10 kwa kuwashirikisha baadhi ya wananchi.

Akasema mafunzo hayo yanayoanzia na kuandaa shamba hadi uvunaji wa zao husika, yanalenga katika kuwafanya wawe wataalamu wa kilimo waliobobea.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.