15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Muafaka: Sasa ni jino kwa jino tu..!
 
2008-05-15 19:55:19
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Ule mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete aliahidi kuushughulikia sasa unaelekea kukua zaidi baada ya vyama hasimu vya CCM na CUF kuendelea kulumbana kwa staili inayoonekana wazi kuwa ni ya siasa zile za `Jino kwa jino!

Hiyo inatokana na ukweli kuwa leo, ikiwa ni siku moja tu baada ya Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM, kumpaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na mwenyekiti wake Professa Ibrahim Lipumba kuwa hawana ufahamu wa kutosha, chama hicho (CUF) kimesema kuwa nacho kinajipanga kujibu mapigo hayo.

Akizungumza kwa simu na Alasiri leo asubuhi, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Bw. Mbarara Maharagande, amesema kuwa tayari chama hicho kimeiagiza Sekretarieti ya Vijana kujibu mashambulizi ya UVCCM.

Akasema miongoni mwa vitu vitakavyojibiwa na vijana hao wa CUF ni pamoja na mazungumzo ya Muafaka, kauli ya UVCCM kuwa wako tayari kwa vurugu, kashfa dhidi ya Seif na Prof. Lipumba.

``Tumeiagiza Sekretarieti ya vijana wetu iwajibu UVCCM, kwa vile tumeona sio utaratibu wa kiprotokali tukiwajibu sisi,`` akasema Bw. Maharagandi.

Katika madai yao yaliyotolewa jana, UVCCM wamedai kuwa mgogoro wa kisiasa visiwani humo umesababishwa kwa kiasi kikubwa na uhuni pamoja na uwezo mdogo wa ufahamu wa Maalim Seif Shariff Hamad mwenye shahada ya Chuo Kikuu Dar na Profesa wa Uchumi, Bw. Ibrahim Lipumba.

UVCCM wamesema katika taarifa yao iliyotolewa na Katibu, Bw. Francis Mtinga, kuwa Seif anamburuza Prof. Lipumba ili akidhi mahitaji yake binafsi.Na Mwandishi Wetu, Jijini.

ULE mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete aliahidi kuushughulikia sasa unaelekea kukua zaidi baada ya vyama hasimu vya CCM na CUF kuendelea kulumbana kwa staili inayoonekana wazi kuwa ni ya siasa zile za \'Jino kwa jino!

Hiyo inatokana na ukweli kuwa leo, ikiwa ni siku moja tu baada ya Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM, kumpaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na mwenyekiti wake Professa Ibrahim Lipumba kuwa hawana ufahamu wa kutosha, chama hicho (CUF) kimesema kuwa nacho kinajipanga kujibu mapigo hayo.

Akizungumza kwa simu na Alasiri leo asubuhi, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Bw. Mbarara Maharagande, amesema kuwa tayari chama hicho kimeiagiza Sekretarieti ya Vijana kujibu mashambulizi ya UVCCM.

Akasema miongoni mwa vitu vitakavyojibiwa na vijana hao wa CUF ni pamoja na mazungumzo ya Muafaka, kauli ya UVCCM kuwa wako tayari kwa vurugu, kashfa dhidi ya Seif na Prof. Lipumba.

``Tumeiagiza Sekretarieti ya vijana wetu iwajibu UVCCM, kwa vile tumeona sio utaratibu wa kiprotokali tukiwajibu sisi,`` akasema Bw. Maharagandi.

Katika madai yao yaliyotolewa jana, UVCCM wamedai kuwa mgogoro wa kisiasa visiwani humo umesababishwa kwa kiasi kikubwa na uhuni pamoja na uwezo mdogo wa ufahamu wa Maalim Seif Shariff Hamad mwenye shahada ya Chuo Kikuu Dar na Profesa wa Uchumi, Bw. Ibrahim Lipumba.

UVCCM wamesema katika taarifa yao iliyotolewa na Katibu, Bw. Francis Mtinga, kuwa Seif anamburuza Prof. Lipumba ili akidhi mahitaji yake binafsi.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.