|
Mteza kusimamia mtihani wa waamuzi
2008-05-16 15:52:13
By Robert Temalilwa, Kinondoni
Mkufunzi wa waamuzi wa soka manispaa ya Kinondoni, Hemed Mteza ameteuliwa kusimamia mtihani wa Taifa ulioandaliwa na Shirikisho la Soka nchini, TFF, kwa ajili ya waamuzi 35 wa wilaya hiyo.
Katibu msaidizi wa Chama cha Waamuzi wilayani Kinondoni, KIFRA, Haji Kalindo, amesema mtihani huo utafanyika Mei 25 kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es salaam.
Kalindo amesema lengo la mtihani huo ni kwa ajili ya kuwaweka sawa waamuzi wa manispaa hiyo ili kuweza kupata waamuzi bora ambao watakuwa katika kiwango kinachokubalika katika taalumu hiyo.
Amesema kufanyika kwa mtihani huo ni utekelezwaji wa mikakati ya TFF ya kuendeleza waamuzi kwa lengo la kupata waamuzi bora wanaokubalika Kimataifa.
Kalindo amesema mtihani huo utawashirikisha waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, waamuzi wa daraja la kwanza, pili na la tatu.
|