16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Manispaa ya Kinondoni yakusanya Sh. Bilioni 5.7
 
2008-05-16 16:02:23
Na Onesmo Kapinga, Kinondoni

Halmashauri ya Manispaa Kinondoni Jijini imekusanya Sh. 5,727,019,901,00 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato, imefahamika.

Aidha, Halmashauri hiyo ililenga kukusanya Sh.8,200,000,00 kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi kufikia Machi 2008 , ambapo badala yake ilikusanya kiasi hicho cha Sh.5,727,019,901,00 ikiwa ni sawa na asilimia 70.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Noel Mahyenga , wakati alipokuwa akizungumza na mwanadishi ofisini kwake.

Akasema makusanyo ya fedha hizo yamesaidia kuboresha miundombinu ya barabara za kata, ikiwa ni pamoja na kutemngeneza barabara za changarawe zenye urefu wa kilomita 87.35 na za kiwango cha lami kwa barabara ya Mtogole yenye urefu wa kilomita 0.15 pamoja na ile ya Idrisa yenye urefu wa kilomita 0.27.

Aidha, akasema wameweza kupanua Mto Ng`ombe uliopo Tandale, ujenzi wa madaraja ya waenda kwa miguu, kufanya ukarabati wa karavati ya Mavurunza mpaka King\'ongo, kukarabati kituo cha mabasi Makumbusho na pia kujenga mifereji ya maji ya mvua katika masoko ya Kawe na Kinondoni.

Akasema kuwa wameweza vilevile kujenga vyumba vya madarasa ya sekondari za kata 21, huku wakiwa wamewashirikisha wananchi, kununua matrela 25 ya kubebea taka, kujenga vizimba na kukarabati mabomba ya maji ya eneo la Mpigi Magoe na kuchimba visima katika maeneo ya Mabibo, Magomeni na Makuti.

Aliongeza kuwa Halmashauri hiyo imeweka mikakati ya kukuza uchumi na kujiongezea pato lake kwa kutoa maeneo ya uwekezaji kwa wawekezaji kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Maeneo yaliyowekwa kwa uwekezaji ni Ufukwe wa Oysterbay, viwanja vya nyumba vya Oysterbay plot N0. 277 na 322, Kituo cha mabasi Makumbusho na maeneo kongwe ya Magomeni,
Akasema lengo ni kuongeza mapato yake ya ndani na kuboresha huduma baada ya kukamilika kwa uwekezaji huo ambao pia utaisaidia jamii.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.