16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanafunzi Chuo cha Ustawi Dar kuuburuza...
 
2008-05-16 16:11:14
Na Abdul Mitumba, Kijitonyama

Wanafunzi 437 wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama wanatarajiwa kuufikisha mahakamani uongozi wa chuo hicho baadaye leo ili pamoja na mambo mengine, kuomba ufafanuzi wa kisheria juu ya vyeti watakavyotunukiwa kuwa ni vya Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma).

Kwa maelezo yao, wanafunzi hao wamedai kuwa kusudio la kwenda kortini limekuja baada ya kutokea kutoelewana kati yao, uongozi wa chuo na Baraza linalosimamia vyuo vya elimu ya juu nchini, NACTE, juu ya kipi wanachosoma wanafunzi hao walioanza masomo mwaka 1995/96, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mchakato wa kukipa hadhi chuo hicho kutoa shahada za kwanza.

Wakizungumza na Alasiri chuoni hapo jana, wanafunzi hao wamesema hatua ya kwenda mahakamani inafuatia kutoelewana baina ya pande hizo tatu na kwamba wataiomba mahakama kuzuia kwanza kufanyika kwa mitihani yao baadaye mwezi ujao.

Wamedai kuwa utata ulizuka baada ya wanafunzi hao kubaini kuna udanganyifu uliofanywa na chuo kuwasaili ili kuchukua Stashahada ya Juu wakati miezi kadhaa nyuma serikali ilichafuta kiwango hicho cha elimu na kupandisha hadi hadhi ya Shahada ya Kwanza.

Kwa mujibu wa tangazo la Serikali Namba 153 lililochapishwa Juni 10 2005 na lile Namba 223 la Agosti 5 2005, inafafanua serikali kukipa hadhi chuo hicho kutoka kutoa elimu ya Stashada ya Juu hadi Shahada ya Kwanza inayotambuliwa na NACTE.

``Wakati serikali ikitangaza hayo, sisi wanafunzi tunaopaswa kumaliza mwezi ujao, tulisailiwa chuoni hapo Oktoba 3 2005 na wakati wote tumekuwa tukisoma masomo yanayotupa haki ya kufanya mitihani ya Shahada ya Kwanza,`` amesema mmoja wa wanafunzi hao.

Wakafafanua kuwa, baada ya kutoelewana kwa muda mrefu, Baraza la Wanafunzi wa Chuo hicho, ISWOSO, likawasiliana na kampuni ya mawakili ya The South Law Chambers chini ya Dk. Sengondo Mvungi ili kuufikisha mahakamani uongozi wa chuo na hatimaye kupata ufafanuzi wa kisheria.

Akizungumza na Alasiri jana, Mkurugenzi wa Mafunzo wa chuo hilo, Bw.Charles Mlwande Madihi, amekiri kuwepo kwa dhamira ya wanafunzi hao na kwamba wapo tayari kusimama kizimbani.

``Siyo kweli kwamba chuo kimefuta elimu ya Stashahada ya Juu... kilichofanyika ni Serikali kukiongezea hadhi chuo hadi kutoa Shahada ya Kwanza, haiwezekani wanafunzi hao wasailiwe kusoma Advanced Diploma halafu wafanye mitihani ya Bachelor Degree?`` Alihoji Bw.Madihi.

Amewataka wanafunzi hao kutumia muda wao mwingi kusoma kwa bidii ili fanye vizuri mitihani yao mwezi ujao, vinginevyo watafeli hivyo kupoteza muda wao bure chuoni hapo.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.