16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ajali mbaya Dar yaua
 
2008-05-16 16:14:06
Na Mwanaididi Swedi, Kinondoni

Ajali mbaya ya gari imetokea Jijini Dar jana na kuua, kujeruhi na pia magari husika kuharibika vibaya.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema tukio hilo limetokea jana, majira ya saa 9:00 alasiri katika barabara ya Mandela, eneo la kituo cha Gereji pale Mabibo.

Akielezea ajali hiyo, Kamanda Rwambow amesema ajali hiyo imetokea baada ya gari namba T 908 ADZ aina ya Toyota Corolla, lililokuwa likiendeshwa na Abdalah Mohamed, 27 kutokea Buguruni kwenda Ubungo, kuacha njia na kuhamia upande wa kulia mwa barabara kabla ya kuzolewa na gari jingine lililokuwa kwenye mwendo wa kasi na kusababisha uharibifu mkubwa wa magari hayo.

Kamanda Rwambow amesema gari hilo liligongana na gari namba T 858 ACK aina ya Toyota Pick-up, iliyokuwa ikiendeshwa na Mohamedi Pazi, 35, aliyekuwa akitokea Buguruni.

Amesema katika ajali hiyo, abiria aliyekuwa kwenye Pick-up Bw. Frank ambaye umri wake haukuweza kuhafahamika mara moja, alifariki papohapo na wengine kujeruhiwa.

Amesema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa juu ya hali za majeruhi wa ajali hiyo na mahala waliko.

Wakatu huo huo, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Demetia Alloyce, 37, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kanga yake.

Kamanda Rwambow amesema mwanamke huyo alikuwa mke wa Bw. Juma Rajabu, 37, mfanyakazi wa Kampuni ya simu ya Vodacom.

Amesema Kamanda Rwambow kuwa mwanamke huyo amejinyonga chumbani kwake wakati mumewe akiwa kazini.

Amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo chake.

Amesema kuwa hadi sasa, Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.