17 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakulima kuneemeka
 
2008-05-17 15:13:39
Na Azizi Issa

Huenda wakulima wakaanza kuneemeka mara baada ya Serikali, kukamilisha ufumbuzi wa tatizo la masoko ya mazao yao.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Bi. Celina Kombani serikali imeanza mchakato wa kutafuta masoko ya mazao yao.

Akasema hatua hiyo inalenga katika kupunguza na kama si kumaliza kabisa tatizo la masoko kwa mazao yao ya kilimo.

Akasema ugumu ambao wamekuwa wakiupata wakulima umekuwa ukiwakwaza katika shughuli za uzalishaji.

Aidha, akizungumzia kuhusiana na kukosekana kwa mbolea za ruzuku katika mkoa wa Tabora, Waziri huyo akasema serekali inakusudia kurejesha utaratibu wa kutoa mbolea ya ruzuku kwa wakulima.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.