17 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mali za viongozi wa Mabatini SACCOS kupigwa mnada
 
2008-05-17 15:42:19
Na Onesmo Kapinga, Tandika

Mali za viongozi wawili wa Chama cha Ushirika, Akiba na Mikopo cha Mabatini SACCOS kilichoko Tandika wilaya ya Temeke, zimekamatwa kwa ajili ya kuzipiga bei kutokana na kushindwa kwao kurejesha mkopo waliokopa kutoka kwenye chama hicho.

Akizungumza na Alasiri Jijini, Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw Said Msonga, amesema mali zilizokamatwa ni pamoja na gari la mjumbe mmoja wa kamati ya usimamizi.

Bw. Msonga akasema gari hilo aina ya Corolla ambalo limekamatwa na dalali wa Majembe Action Mart, linatarajiwa kuuzwa baada ya kwisha kwa notisi aliyopewa ya wiki mbili ya kulipa deni hilo ili lisiuzwe kufidia fedha alizokopa.

Akasema kuwa kukamatwa kwa gari hilo kunatokana na kushindwa kurejesha mkopo wake kwa muda waliokuwa wamepangiana.

Bw. Msonga akasema kuwa mjumbe huyo alikopa Sh. 7,320,000 na alitakiwa kurejesha Sh.10, 870, 000, ikiwemo na riba ya Sh. 3,450,000.

Aidha, akamtaja mdaiwa mwingine kuwa ni kiongozi wao mmoja aliye miongoni mwa wale wa ngazi za juu anayedaiwa Sh. Milioni 30.

Akasema gari la kiongozi huyo, pia liko hatarini kukamatwa na kupigwa mnada kwani alikopa sh. milioni 20,395,000 na kutakiwa kurejesha na riba ya Sh. Milioni 9.7.

Bw. Msonga akasema vilevile kuwa gari aina ya Nissan Patrol la mwanachama wao mwingine nalo limekamatwa na dalali, akidai kuwa naye ameshindwa kurejesha sh. milioni 9.

Akasema kuwa chama chicho kinawadai baadhi ya wanachama zaidi ya sh. milioni 89 na hivyo kusababisha huduma ya utoaji wa mikopo kwa wateja wengine kusimamishwa.

Bw. Msonga kuwa huduma hiyo ilisitishwa ili kuelekeza nguvu kwa wadaiwa sugu ambao wameshindwa kurejesha fedha chama kwa muda uliokwa umepangwa.

Hata hivyo, akasema kuwa pamoja na kuwavumilia kwa muda mrefu, wadaiwa hao wameshindwa kutoa sababu za msingi na hivyo kuwalazimu kufikiria namna ya kufilisi mali zao ili kufidia pesa walizokopa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.