|
Maslahi duni yawakimbiza wahandisi...
2008-05-17 15:49:34
Na Onesmo Kapinga, Jijini
Serikali imeshauriwa kuinua pato la wahandisi nchini ili hatimaye waweze kuwavutia kwa vijana wengi kujiunga na fani hiyo ambayo kwa sasa ina uhaba wa wafanyakazi.
Aidha, vijana wengi wanaikimbia fani hiyo kutokana na ugumu wa masomo ya sayansi, pamoja na kuwa na pato dogo ambalo halina maslai mazuri kwa mfanyakazi.
Hayo yamesemwa na Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini, Bw. Steven Mlote, alipokuwa akizungumza na Alasiri ofisini kwake.
Akasema hivi sasa wanakabiliwa na uhaba wa wahandisi nchini kutokana na ukweli kuwa vijana wengi wanaikwepa fani hiyo kutokana na ugumu uliopo na maslai madogo.
``Nafikiri kama Serikali ikijaribu kuboresha maslai ya mfanyakazi, wasomi wengi watajiunga kusomea uhandisi kwa itakuwa ikiwavuti`` alisema Bw. Mlote
Alisema kwa sasa hapa nchini kuwa wahandisi 8,000 tu na makapuni yaliyopo ni 29 ya kigeni na ya ndani 106.
Aidha, akaongeza kuwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi imeanza kampeni ya kukagua makampuni ya wahandisi na makandarasi wote wa daraja la kwanza hadi la tano, kwa kuhakikisha kuwa utendaji kazi wao unalingana na viwango vya usajili walivyopatiwa.
Akasema ukaguzi huo pia utahusisha makampuni yote yanayotoa ushauri wa kihandisi na kuhakikisha kama wanawahandisi wenye uwezo wa kutoa ushauri bora.
Akasema makampuni mengi ya makandarasi nchini hayana wahandisi wenye sifa na wamekuwa wakitumia vigezo mbalimbali ili weweze kusajiliwa, huku wakiwa hawana sifa za kutosha katika ngazi za madaraja wanayoombea usajili.
Bw. Mlote akasema hali hiyo inasababisha wahandisi wengi kufanya kazi zao pasipokuwa na kiwango kizuri na kuleta hasara ya kubomoka kwa majengo mengi, ama uchakavu wa barabara kwa haraka.
Aidha, Bw. Mlote akasema makampuni yote ya makandarasi na wahandisi yatakayobainika kuwa hayafikii viwango, yatafutiwa usajili na kuchukuliwa hatua zaidi kwa mujibu wa sheria.
Akasema hadi sasa, makampuni matano yamefutiwa usajili kutokana na kutokuwa na wahandisi wenye viwango bora ambapo kati ya hayo, manne ni ya kigeni na moja ni la hapa nchini.
Akayataja makampuni yaliyofutiwa kuwa ni pamoja na BKS Global LTD lenye usajili wa namba 026 la Dar es Salaam, Wgs Consultants N0.009 toka Arusha, Japan Engineering Consultants N0.022 lililopo Mto wa Mbu, Parkman N0.023 Dar es Salaam, na Tangroup N0.024 la Dar es Salaam.
Akasema kutokana na mujibu wa sheria ya usajili wa wahandisi ya mwaka 97 na kama ilivyolekebishwa mwaka 2007 , inasema kampuni zote za kihandisi zikifutwa, pia wahandisi wao washauri hufutwa.
Bw. Mlote amesema kutokana na sheria hiyo, wahandisi watatu waliokuwa wakitoa ushauri katika makampuni hayo walifutwa ambo ni Suleiman Rashid, Testuro Izawa na Stuart Herderson.
|