06 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Madonna amekanusha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari
 
2006-10-06 15:58:21
Na EAR Habari

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa pop wa Marekani, Madonna, amekanusha taarifa zilizotolewa na vymbo vya habari, kwamba na mpango wa kutaka kuchukua Mtoto wa kiume kwa nia ya kumlea, nchini Malawi.

Akiongea na shirika la Habari la AP, msemaji wa mwanamuziki huyo Liz Rosenberg, amesema kwamba mwanamuziki huyo hajachukua mtoto wa kiume, kama taarifa za hapo awali zilivyodai, ambapo amedai kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Rosenberg amesema kwamba Mwanamuziki huyo yuko nchini Malawi kwa ziara binafsi, ambapo anashiriki katika ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima, pamoja na mipango mingine ya kusaidia watoto, waliopoteza wazazi wao kutokana na ugonjwa wa ukimwi.

Hivi karibuni Maafisa wa serikali ya Malawi, walidai kwamba Madona yuko katika harakati za kutuma maombi, ya kuchukua mtoto wa kiume nchini humo.

  • SOURCE: EAR
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.