|
Wanafunzi 3 wamekufa baada ya kufunikwa na mchanga
2006-10-25 14:48:40
Na EAR Habari
Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Kilanga-langa, wilayani Namtumbo, Mkoani Ruvuma Nchini Tanzania, wamekufa baada ya kufunikwa na mchanga, na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Fulham Mshana, amesema watoto hao walipatwa na tukio hilo, wakati wakichimba mchanga wa kujenga nyumba, kazi ambayo walipewa na mjenzi wa nyumba hiyo.
Kamanda Mshana, ameyataja majina ya watoto hao waliokufa, kuwa ni Ismail Hocho, Furahya Komba, na Sophia Mbawala.
|