|
Kipindupindu chauwa wafungwa wanne Uganda
2006-12-31 15:44:40
Na EAR Habari
Wafungwa wanne katika gereza la Kabasanda wilayani Mpigi nchini Uganda wamekufa, kutokana na ugonjwa wa kipindupindu uliolikumba gereza hilo.
Kwa mujibu wa mkuu wa gereza hilo, Bw. Lawrence Buserezi mmoja wa wafungwa hao amekufa akiwa njiani kuelekea nyumbani baada ya kumaliza kifungo chake.
Hata hivyo vyanzo vya habari nchini Uganda vimedai kwamba chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo katika gereza hilo ni msongamano uliopo gerezani hapo, pamoja na hali ya uchafu iliyokithiri.
|