|
Kamishna wa Jeshi la Polisi Kenya ametakiwa kujiuzulu
2007-04-29 15:04:27
Na EAR Habari
Waziri Msaidizi wa Wanyamapori nchini Kenya, Mh. Kalembe Ndile, amemtaka Kamishna wa Jeshi la Polisi, Meja Jenerali Hussein Ali, kujiuzulu, kutokana na kuzorota kwa usalama katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.
Mh. Ndile ametoa wito katika mkutano wake na waandishi wa habari, kufutia kuwepo kwa shinikizo la kumtaka bosi huyo wa Jeshi la polisi Kenya, ajiuzulu, kwa kushindwa kudhibiti uhalifu.
Amesema jeshi la polisi halina sababu za kujitetea kutokana na kuzorota kwa amani nchini Kenya, kwa kuwa serikali imetumia mabilioni ya shilingi, ili kuliwezesha kukabiliana na uhalifu.
|