|
Mahabusu wapatao 10,040 wanashikiliwa Uganda bila kesi zao kutajwa
2007-04-29 15:05:07
Na EAR Habari
Habari kutoka Uganda, zinasema kuwa mahabusu wapatao 10,040, wanashikiliwa magerezani, kwa muda mrefu, bila ya kesi zao kutajwa mahakamani.
Taarifa zaidi zimesema, mamia ya mahabusu nchini humo, wapo kizuizini kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja hadi mitano, bila ya kesi zao kufikishwa mahakamani.
Miongoni mwa mahabusu hao, ni wanaokabiliwa na kesi za mauaji, kesi za wizi, kesi za ulawiti, ubakaji, uhalifu mdogo mdogo, pamoja na kesi za mauaji yasiyo kusudiwa.
|