|
Jeshi la Sudan limeikosoa ripoti ya Umoja wa Mataifa
2008-03-23 15:12:57
Na EAR Habari
Jeshi la Sudan limeikosoa ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa, iliyolishutumu jeshi hilo kuhusuka na vitendo vya kubaka wanawake na wasichana, na kuvamia na kupora katika miji wakati wa mashambulizi huko magharibi katika jimbo la Darfur.
Msemaji wa jeshi la Sudan pia amekanusha ripoti za Umoja wa Mataifa, kuwa uvamizi uliofanya kwa njia ya anga na majeshi ya ardhini katika miji mitatu mnamo mwezi februari, ulisababisha vifo vya watu 115.
Brigedia Jenerali Osman Mohamed al-Aghbash, amesema jeshi linatekeleza wajibu wake wa kuwalinda raia kwa kuwafukuza waasi.
Aidha amewalaumu waasi wa huko Darfur kwa kuwashambuliwa raia, na kupora mali zao.
|