|
WHO hawana taarifa na utengenezwaji wa ARV Tanzania
2008-03-23 15:13:35
Na EAR Habari
Shirika la Afya Duniani WHO, limesema halina taarifa za kutengenezwa kwa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARVs, zinazoanza kutengenezwa nchini Tanzania kwa niaba ya serikali.
Msemaji wa Shirika hilo kwenye ofisi zake zilizoko Dar es Salaam, amesema wamefahamu kuhusu kutengenezwa huko kwa dawa hizo, kupitia vyombo vya habari vya ndani.
Kauli hiyo ya WHO imekuja baada ya mtengenezaji wa ndani wa dawa hizo kwa majaribio, kudai kuwa ametuma maombi kwa Shirika hilo akitaka kiwanda chake kukaguliwa, lakini hajapewa majibu mpaka sasa.
|