23 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Migogoro binafsi ya mawaziri wa afya wa Uganda yaathiri utendaji
 
2008-03-23 15:14:10
Na EAR Habari

Imeelezwa kuwa migogoro binafsi ya malumbano baina ya mawaziri wa afya wa Uganda, imeathiri utendaji wa maafisa wengine katika idara za afya, na kuathiri utoaji huduma za afya nchini humo.

Baadhi ya athari za malumbano hayo zimetajwa kuwa ni pamoja na kujitoa kwa baadhi ya wafadhili kutoa misaada ya kifedha, kwa sababu ya kutoridhishwa na usimamizi wa miradi wanayofadhili.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya nchini Uganda Dakta Sam Zaramba, amesema wakati mwingine baadhi ya maafisa katika makao makuu ya wizara ya afya wanakwenda kinyume na utaratibu, na kutotekeleza kanuni za usimamizi wa fedha zilizowekwa na serikali.

  • SOURCE: EAR
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.