23 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wazazi Kenya wataka kuanzishwa kwa bodi ya mitihani
 
2008-03-23 15:15:35
Na EAR Habari

Chama cha Taifa cha Wazazi nchini Kenya kimeliomba Baraza la Taifa la Mitihani nchini humo, kuanzisha bodi ya mitihani.

Chama hicho cha Wazazi kimesema utendaji wa baraza hilo umeingia dosari, kutokana na namna baraza hilo lilivyosimamia mitihani ya kumaliza elimu ya sekondari
Nchini humo mwaka jana.

Wito huo wa chama cha wazazi umetolewa kufuatia kutakiwa kutolewa upya kwa matokeo ya mitihani ya zaidi ya wanafunzi elfu 4, kwa kile baraza la taifa la mitihani lilichokiita kukosewa kwa gredi zilizotolewa.

  • SOURCE: EAR
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.