|
Shule ya biashara Makerere yalumbana na wizara yab elimu
2008-03-24 16:52:57
Na EAR Habari
Shule ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, imeingia katika malumbano na wizara ya elimu kuhusiana na utaratibu wa uteuzi wa wafanyakazi wake.
Shule hiyo inaishutumu wizara kupitia tume ya watumishi wa elimu, kwa kutangaza nafasi ya naibu makamu wa chuo bila ya kuhusishwa.
Baraza la shule hiyo limepinga tangazo la ajira lililotolewa na wizara, kwa madai kuwa jukumu hilo ni lao, kwani makamu huyo wa shule ya biashara atakuwa muajiriwa wao.
|