|
Marekani yalegeza tahadhari ya raia wake kutosafiri Kenya
2008-03-24 16:54:42
Na EAR Habari
Marekani imetoa taarifa ya kulegeza tahadhari ya kuto safiri nchini Kenya, ambayo imeeleza kuwa ghasia zimepungua mno nchini humo, baada ya kufikiwa makubaliano ya kugawana madaraka.
Taarifa hiyo imepokelewa vyema na sekta ya utalii ya Kenya, ambayo imeanza kuzaa matumaini ya kupata watalii zaidi kutoka Marekani.
Hata hivyo taarifa ya tahadhari ya usafiri, imewaonya raia wa Marekani watakaotembelea Kenya kuwa waangalifu, ili kuepuka uwezekano wa kukabiliwa na vitendo vya uhalifu.
|