|
MDC bado hawajafikia maamuzi ya kurudia uchaguzi
2008-05-04 23:13:41
Na EAR Habari
Chama cha upinzani cha Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC, kimesema bado hakijafikia maamuzi iwapo kitashiriki uchaguzi wa marudio ama hakitashiriki.
Ujumbe wa chama hicho unatarajiwa kutembelea Afrika Kusini, kuonana na kiongozi wa chama hicho Bw. Morgan Tsvangia, kabla uamuzi wa mwisho haujatolewa.
Mpaka sasa Bw. Tsvangirai hajadhibitisha kushiriki uchaguzi huo, hatua ambayo moja kwa moja iwapo hatashiriki itampa ushindi rais wa sasa Bw. Robert Mugabe.
|