|
Walimu nchini Zimbabwe wakimbia na kusababisha baadhi ya shule kufungwa
2008-05-08 14:26:11
Na EAR Habari
Vitendo vya vurugu ambavyo vinazidi kuongezeka nchini Zimbabwe, kufuatia uchaguzi mkuu nchini humo, vimesababisha waalimu maeneo ya vijijini ambao wengi wao walikuwa wakala wa uchaguzi, kukimbia na kusababisha baadhi ya shule kufungwa.
Chama cha waalimu nchini humo kinakadiria kuwa, zaidi ya waalimu 1000 wamepigwa na wanamgambo ambao wanasadikiwa kuwa wa chama tawala, na zaidi ya shule 100 kufungwa.
Katibu Mkuu wa Progressive Teachers Union of Zimbabwe Raymond Majongwe, amekaririwa akisema kwamba jambo linalosikitisha ni kwamba mwezi juni unakaribia, kwa wanafunzi kufanya mtihani, na hakika watashindwa kwa sababu hakuna waalimu.
|